Hatimaye Zanzibar Yapiga Marufuku Nyama ya Kasa

 

Zanzibar yapiga marufuku nyama ya kasa

Serikali kupitia Wizara ya Afya Zanzibar imewataka wananchi kuacha kula nyama ya kasa ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo kifo. - Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari huko Ofisini kwake Mnazimmoja, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hassan Khamis Hafidh amesema hatua hiyo imekuja kufuatia vifo vya watu tisa na wengine 18 kulazwa katika Hospitali ya Abdalah Mzee kati ya watu 160 waliokula nyama hiyo inayosadikiwa kuwa na sumu. - Akitoa taarifa ya kitaalam Mkemia Mkuu wa Serikali ya Zanzibar, Faridi Mzee Mpatani amesema kitaalamu kuna aina saba za kasa ambapo katika aina hizo, aina nne za kasa kuna baadhi ya vyakula wakila wanadamu humsababishia maradhi ama kifo. - Ameeleza kuwa kwa kushirikiana na Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ya Tanzania Bara, wamefanya uchunguzi wa kitaalamu na kubaini uwepo wa sumu katika nyama hiyo na kusema kuwa sumu hiyo inahimili joto ambapo hata ikipikwa haiwezi kuondoka. - Aidha ameongeza kuwa sumu hiyo kitaalamu inajuulikana kwa jina la telenikostizim ambayo husababisha madhara katika mfumo wa mwanadamu ikiwemo kuhisi kichefuchefu, homa na baadae kufariki. - Itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 6 Machi kuliripotiwa taarifa za tukio hilo lililotokea katika Kisiwa Panza Mkoa wa kusini Pemba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad