Hichi Hapa Kikosi Kipya Cha Taifa Stars, Sababu ya Mbwana Samatta Kutemwa




Shirikisho la soka nchini (TFF) limetoa taarifa ya sababu za Nahodha wa timu ya Taifa Stars,' Championi Boy' Mbwana Samatta kutoitwa kwenye kikosi kinachoelekea kwenye mashindano ya FIFA Series 2024.

"Nahodha wa Stars, Samatta ameomba kutojumuishwa kwenye kikosi kwa michezo ya FIFA Series na alizungumza na kocha kabla ya kutajwa kwa kikosi hicho na kuomba ombi hilo ambalo limekubaliwa," imesema taarifa hiyo.

Kikosi cha wachezaji 23 kilichoitwa leo na Kaimu Kocha Mkuu, Hemed Suleiman 'Moroco' kwenye eneo la washambuliaji kimemwacha nahodha Samatta na kuwaita Clement Mzize (Yanga), Saimon Msuva (Al najmah FC, Saudia), Kibu Denis (Simba), Abdul Suleiman (Azam FC), Ben Starkie(Likeston Town, Uingereza) na Charles M'mombwa (Macarthur FC, Australia).

Makipa ni Aishi Manula (Simba), Aboutwaleeb Mshery (Yanga), Kwesi Kawawa (Syrianka FC, Sweden) huku mabeki Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Hamad (Yanga), Mohamed Hussein na Kennedy Juma (Simba), Novatus Dismas (Shakhtar Donestsk, Ukraine), Miano Danillo (Villena) na Haji Mnoga wa Aldershot Town ya Uingereza.

Eneo la Viungo kuna Feisal Salum na Yahya Zayd wa Azam FC, Mudathir Yahya (Yanga), Morice Michael (RFK Novi Sad, Serbia), Himid Mao (Tala'ea El Gaish SC, Misri) na Tarryn Allarakhia anayekipiga Wealdstone, Uingereza.

Kikosi hicho kitaingia kambini machi 17, 2024 na kitaondoka Machi 18. Kitacheza michezo miwili na Bulgaria na Mongolia michezo machi 22 hadi 25.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad