Huyu Hapa Mrembo Kutoka Czech Aliyeshinda Miss World 2024

 Mrembo kutoka Czech ashinda Miss World 2024« NyumaMbele »Comments (0)Listen to Article

 


Mwanadada Krystyna Pyszkován kutoka nchini Czech Republic ameshinda taji la Miss World 2024.


Fainali ya mashindano imefanyika jioni ya leo Machi 9, 2024 katika Jiji la Mumbai nchini India yalikokuwa yakifanyika mashindano hayo.


India iliandaa shindano la 71 ambapo washiriki kutoka nchi 115 walikuwa wakichuana kila mmoja akiwa na ndoto ya kurudi na taji hilo nchini mwake.


Miss Tanzania 2022, Halima Kopwe alikuwa miongoni mwa washiriki wa shindano hilo ambapo alitinga kumi bora katika kipengele cha ‘Beauty with Purpose Project’.


Taji hilo mwaka jana Miss World 2022 lilienda kwa Karolina Bielawska wa Poland ambaye mrithi wake Krystyna Pyszková amepatikana leo.


Waliomaliza 'top four' 1. Krystyna Pyszková wa Jamhuri ya Czech 2. Yasmina Zaytoun wa Lebanon 3. Aché Abrahams wa Trinidad 4. Lesego Chombo wa Botswana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad