Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Jemedari Said amemvaa Haji Manara baada ya kumsifia mtangazaji wa soka wa Azam TV, Gharib Mzinga.
Jemedari amesema kuwa alichokifanya Manara ni jitihada zake za kutaka kumshusha mtangazaji Baraka Mpenja huku chanzo kikidaiwa kuwa ni ugomvi kati ya Manara na Mpenja.
"Alikuja Mwamba wa Umarila Baraka Mpenja 'Sauti ya Radi' amekuwa kinara wa utangazaji wa soka kizazi cha 2010+ huku, amekua akifurahisha watu kwa kipindi kikubwa kutokana na namna anavyotangaza mpira.
"Badae kaibuka kilwa Finest Gharib Mzinga ambaye asili yake ni Zanzibar kajijengea jina lake tofauti na Baraka Mpenja. Ni aina ya watangazaji wa miaka ya nyuma, yani anakupa takwimu zilizotokana na utafiti wake. Amejizolea sifa tofauti na za Mpenja na amekua akikua kwa kasi sana.
"Juzi juzi kaibuka KALIKONJI akimsifia sana Mzinga na kujaribu kumponda Baraka kisa eti Baraka Mpenja akitangaza anasifia sana Simba na Chama, so kwenye Group lao moja huo ukawa mjadala na yeye akachukua jukumu la kuazimia kumshusha Mpenja kwa kumuinua Mzinga na kusema Mpenja ni CHAWA. Lakini yote baada ya Azam FC kuichapa Yanga 2-1 Taifa na Mpenja akaitangaza.
"Nikaamua kufuatilia kuona nini kipo nyuma yake, kumbe KALIKONJI kaanzisha na Mpenja baada ya kusikia mtangazaji 1 wa Online TV yake anaitwa Pablo ameaga na kusema anataka kwenda MPENJA TV", amesema Jemedari Said.