Kibu Denis na Mzamiru Yassin Wapigwa Faini Kisa Imani za Kishirikina


Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania leo imetangaza adhabu kwa Wachezaji na Timu mbalimbali za Ligi Kuu ambapo Wachezaji wa Simba SC Kibu Denis na Mzamiru Yassin waliopigwa faini ya Tsh milioni 1 kila mmoja kutokana na kufanya vitendo vilivyoashiria imani za kishirikina.

“Kwenye mechi ya Coastal Union FC 1-2 Simba SC, Wachezaji Kibu Denis na Mzamiru Yassin wa klabu ya Simba wametozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kila mmoja kwa kosa la kuonekana wakiondoa taulo la mlinda mango wa klabu ya Coastal Union, Ley Matampi lililokuwa limewekwa pembeni ya lango wakati mchezo”

“Jambo hilo liliashiria imani za kishirikina, adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 41:5 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad