Kifo Cha MR Ibu Majanga Matupu, Mke Mdogo Naye Ataka Kuongeza Makalio Kwa Fedha za Michango



Mke huyo wa pili wa Mr.Ibu(62) atajwa kujaa tamaa za wazi wazi hadi kwenye pesa za michango ya matibabu ya mumewe

Imeelezwa baada ya kuona mumewe kachangiwa mamilioni ya pesa za matibabu bila kujali hali ya afya ya mumewe sio nzuri, Stellah Marris(33) bado akataka kupewa kiasi cha pesa za michango ya matibabu za mumewe ili akaongeze ukubwa wa makalio kwa sajari, anunuliwe iPhone 15 na kutaka pia anunuliwe gari la kutembelea

Hiyo tisa, kumi mke huyo wa pili imedaiwa kila alipokuwa akienda hospitali kumjulia hali mumewe ni lazima kwanza avae kigodoro ili aonekane ana shepu

Mke huyo imeelezwa alisema yeye bado ni msichana hivyo anahitaji kuhudumiwa na mume ili aonekane mwenye kupendeza na kuvutia japokuwa Mr.Ibu alikuwa anaumwa na akiba yote ya kipesa aliyokuwa nayo alimaliza hadi kufikia kuomba michango ya matibabu kwa mashabiki na wasamaria wema

Kwa mujibu wa chanzo kilichokuwa kikitoa updates za afya ya Mr.Ibu mara kwa mara hiyo ndio sababu kuu mke huyo wa pili alinyimwa uhuru wa kuingia katika akaunti yenye pesa za michango ya matibabu ya mumewe hivyo Stellah kuingia katika mkwaruzano wa bifu la wa wazi na Jasmine mtoto wa kuasili wa Mr.Ibu ambaye na yeye anatajwa kuwa mdada wa mjini aliyetumia kila njia kuingia kwenye akaunt ya pesa za michango.

Mke wa pili alimshutumu Jasmine kutembea kimapenzi na baba yake ila watoto wa kiume wa mke wa kwanza walikana skendo ya baba yao kulala na Jasmine ambaye sasa kajimilikisha kinguvu tiktok ya Mr.Ibu

Jasmine na mtoto wa kiume wa damu wa Mr.Ibu walikamatwa na polisi kwa mahojiano baada ya kutajwa kudukua mifumo ya kipesa na kuiba zaidi ya shilingi milioni 100 kutoka kwenye sehemu ya pesa alizochangiwa baba yao na watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wakati bado anaumwa kabla hajafariki jana

Kwa upande mwingine, mke wa kwanza wa Mr.Ibu baada ya kuachana na yeye imeelezwa aliondoka na kila kitu hivyo kumlazimu Mr.Ibu kuanza maisha upya baadaye ndio akamuoa Stellah Marris mwaka 2015

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad