Kamwe amesema hayo baada ya Ahmed kuiponda Yanga kwa kuweka kiingilio bure kwenye mchezo wao dhidi ya Mameldi Sundowns ambapo amemtaka azungumzie mechi yao dhidi ya Al Ahly na si Yanga kama ambavyo amekuwa akifanya.
“Kila mtu azungumzie mechi yake jamani, sisi hatutaki kumpeleka mtu mjini, kila mtu abaki na mechi yake. Sasa hivi kila wakizungumza kidogo wanaitaja Yanga, tajeni Al Ahly mnaecheza nae, kama sisi tunavyoimtaja Masandawana, tajeni mtu wenu kwa nini mnatufuata fuata sisi? Nyie mnacheza na Al Ahly sio Yanga.
“Sisi Yanga tangu tumeanza hamasa tunamtaja Mamelodi tu, mmeshanisikia mimi nazungumza kuhusu Simba? Nazungumza Mamelodi kwa sababu ndiyo timu tunayocheza nayo. Lakini mtu anaona mechi yake imebuna anawaza aibukie wapi, anaanza kuitaja Yanga, mmeshachelewa.
“Mimi sitaki kumpeleka mtu mjini na sitaki mtu anipeleke mjini, kila mtu azungumzie mechi yake tuone. Tafuta njia yako. Sisi sasa hivi kila mtu simu zinaita, tunaongea na Wasauzi tunawaita hapa kwa Mkapa, na wewe wapigie Waarabu kama una ubavu huo, ongea nao, waite usituingize sisi.
“Serikali imesema tupambane na maaduni jamani, tusipigane wenyewe, wewe si uongee na Mwarabu mnashindwa nini? Mbona sisi tunajiamini tunaongea na Masandawana kwa kujiamini kwamba anakufa kwa Mkapa.
“Lakini mtu anajitokeza anasema wameweka viingilio bure, inkuhusu nini? Kwani mnacheza na sisi? Sisi tunaweza kuweka viingilio bure hata kwenye dabi tukiamua kwa sababu tunaamua wenyewe. Na wewe zungumzia jambo lako usituguse guse sisi, sisi tuna-focus kuifurahisha nchi, mambo makubwa tunataka kuyafanya Jumamosi, mtuache tupumzike tuna kazi kubwa,” amesema Kamwe.