Kocha wa Mamelod Aanza Kuweweseka Juu ya Kupangiwa na Yanga Robo Fainali



Kocha wa @sundownsfc Rhulan Mokwena ameizungumzia @yangasc siku ya jana mara baada ya mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya super sport kumalizika,Rhulan Mokwena aliulizwa juu ya Draw ya Robo fainali na haya yalikuwa majibu yake

"Nimeitazama Draw lakini sina haraka Sana Kwa sababu nimewatazama wapinzani wangu Wote vizuri, nimetazama michezo yote kwenye ligi ya mabingwa na nimetazama kama kocha na sio Mchambuzi hivyo siwezi kuwa na hitimisho lolote. Lakini Kwa bahati nzuri tunakwenda kwenye mapumziko ya FIFA, Hapo sasa maandalizi yangu na akili yangu yote itakuwa Juu ya Yanga"

"Na Nitakwenda mbali zaidi ya nitakavyo weza kufatilia Profile Yao, najua wanakocha mzuri Miguel Gamondi ambaye miaka kadhaa nyuma alipita hapa Mamelod lakini pia wanatimu nzuri , yenye muundo mzuri hivyo tusubiri Kabla sijatoa hitimisho lolote

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad