Lakred, Manula Wana Vita yao Simba

Lakred, Manula Wana Vita yao Simba


Ubora wa kipa Ayoub Lakred kwa sasa kwenye kikosi cha Simba umeanza kuwafanya mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi kuwa na amani juu ya usalama wa lango lao hata wakati ambao amekuwa alikosekana Aishi Manula ambaye kwa kipindi kirefu hakuwa na mpinzani wa kugombea naye namba kikosini.


Tofauti na misimu kadhaa nyuma, kwa sasa imeanza kuonekana kawaida kwa Munula kukaa benchi kutokana na kile ambacho amekuwa akikifanya Lakred ambaye amekuwa msaada Simba kwa kuokoa michomo ya ana kwa ana akifanya hivyo mara tatu dhidi ya Singida Fountain Gate, nne dhidi ya JKT Tanzania na mbili walipokabiliana na Coastal Union.


Licha ya kutoonekana wazi kama ndiye kipa namba moja kwa sasa, lakini ndiye ambaye ametumika zaidi kwenye michezo ya hivi karibuni hasa upande wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo amecheza mechi saba akiruhusu mabao matano na hajaruhusu bao 'clean sheet' kwenye michezo mitatu. Manula amepata nafasi mara moja dhidi ya ASEC Mimosas na hakuruhusu bao.


Kwa mujibu wa takwimu za mechi za hivi karibuni hasa Ligi ya Mabingwa Afrika, Lakred ana asilimia 88 ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza huku Manula akiwa na asilimia 13 na kwa upande wa Ligi Kuu mzani unaonekana kuwa sawa kwa makipa hao tangu Tanzania One alirejea kikosini baada ya kupona majeraha.


Tofauti na timu nyingine ambapo imekuwa ikifahamika kipa namba moja kwenye vikosi, kwa Simba unaweza kuumiza kichwa na hapa kocha wa makipa wa timu hiyo, Daniel Cadena anaeleza ubora wa makipa hao huku akiamini ushindani kati yao utaongeza chachu ya kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali.


"Tumekuwa na mechi nyingi ndani ya kipindi kifupi. Kwa hiyo benchi la ufundi limekuwa likifanya mgawanyo wa nafasi kwa wachezaji ili kutunza nguvu ya kuendelea kupambana kwenye michezo mingine. Wote ni makipa wazuri ambao muda wote wanaonekana kuwa tayari kutumika," amesema kocha huyo.


MANULA KWENDA AZAM? Waswahili wanasema "lisemwalo lipo na kama halipo basi lipo njiani laja", na miongoni mwa mambo ambayo yanazungumzwa kipindi hiki ambacho Manula anakumbana na changamoto ya namba kikosini Simba ni pamoja na uwezekano wa kurejea Azam FC.


Wadadisi wa mambo tayari wanaona uwezekano wa hilo kutokea na ni kama Simba ilisoma mapema alama za nyakati ndio maana iliamua kutafuta kipa mwingine wakati Manula akiwa majeruhi ili kujiandaa na maisha ya bila nyota huyo.


Kwa takribani misimu mitatu Manula amekuwa akihusisha na Azam FC - timu aliyoishi na kuitumikia kwa muda mrefu kabla ya kuhamia Simba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad