Marubani wa Ndege Wasinzia Ndege Ukiwa Angani....



Mamlaka za Indonesia zinachunguza tukio la marubani wa shirika la ndege la Batik kulala usingizi wakati wakiwa hewani kwa dakika 28.

Marubani hao ambao wamesimamishwa kazi kwa muda, walisinzia na kulala wakiwa kwenye safari kutoka Sulawesi kwenda mji mkuu Jakarta, Januari 25.

Mmoja wa marubani hao inadaiwa alikuwa amechoka kutokana na kumhudumia mkewe nyumbani ambaye alikuwa amejifungua mapacha.

Ndege hiyo aina ya Airbus A320 ilipoteza mwelekeo kidogo, lakini ilitua salama ikiwa na abiria wake 153 pamoja na wahudumu.

Taarifa zinasema rubani mmoja, 32, alimuomba rubani msaidizi aendeshe ndege nusu saa baada ya ndege kupaa, akisema anahitaji kupumzika kidogo. Rubani wa pili, 28, alikubali jukumu hilo, kwa mujibu wa wizara ya usafiri ya Indonesia.

Lakini rubani huyo msaidizi naye alisinzia na kulala. Taarifa zinasema mke wa rubani huyo alikuwa amejifungua mapacha na alikuwa akisaidia katika kuwahudumia.

Mnara wa mawasiliano ya ndege wa Jakarta ulijaribu kuwasiliana na ndege hiyo, lakini hawakupata majibu yoyote.

Mawasiliano yalisita kwa dakika 28, hadi rubani mkuu alipozinduka na kubaini kuwa rubani msaidizi naye amelala fofofo. Alirekebisha pia mwelekeo wa ndege.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad