Wanasayansi kusema wamefanikiwa kuondoa Virusi vya Ukimwi kutoka kwenye chembechembe zilizoambukizwa.
Wanasayansi hao wanasema wametumia teknolojia ya uhariri wa jeni ya Crispr iliyoshinda Tuzo ya Nobel.
Inafanya kazi kama mkasi, lakini katika kiwango cha molekuli, hukata DNA ili chembechembe"mbaya" ziweze kuondolewa au kuzimwa.
Matumaini ni kwamba inaweza kuondoa kabisa virusi mwilini, ingawa kazi zaidi inahitajika ili kuangalia kama itakuwa salama na yenye ufanisi.
Dawa zilizopo za VVU zinaweza kuzuia virusi lakini sio kuviondoa.