Miaka 20 Jela Kisa Vipande 14 vya Nyama ya Pofu

Miaka 20 Jela Kisa Vipande 14 vya Nyama ya Pofu


Mahakama ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jela Kijana Mussa Ally Makandaje (32), Mkazi na Kijiji cha Msinjili Wilaya ya Tunduru baada ya kupatikana na hatia katika kosa la kukutwa na vipande 14 vya nyama ya mnyama aina ya pofu.


Akisoma hukumu hiyo ya kesi ya jinai Na.18 ya mwaka 2023, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Lilian Haule amenukuliwa akisema “Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo kuacha shaka yoyote”.


Imeelezwa kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo August 10 2023 na kufikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza August 25 2023.


Pofu ni Mnyama Jamii ya swala anayepatikana katika mbuga mbalimbali za Tanzania na anatajwa kuwa na mwili mkubwa kuliko wote katika Jamii hiyo ya swala, sifa nyingine ni sura nzuri pamoja na utamu wa nyama yake uliyoifanya kuwa moja ya nyama zinazopendwa sana katika uwindaji

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad