.
"Hospitali ya Taifa Muhimbili ina vitanda vinavyotosheleza kabisa kukidhi mahitaji ya wagonjwa wote walipo hospitali, lakini kilichotokea katika video fupi ni kwamba kama hospitali tuna utaratibu wa kufanya usafi, ni bahati mbaya imetokea kwamba wakati tunafanya usafi Wamama walichagua kama ilivyo utamaduni wetu kuweka mkeka chini na kukaa. Lakini kwa ujumla kilichotokea tulikuwa tunafanya usafi". Amesema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Julieth Magandi.
Dkt. Magandi alikuwa akitoa ufafanuzi kuhusu picha ya video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha watoto wanalala chini hospitalini hapo kwa madai ya kukosa vitanda.
Ametoa ufafanuzi huo mkoani Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na waandishi wa habari.