Mwigulu Awasilisha Mapendekezo Haya Bajeti Kuu

Mwigulu Awasilisha Mapendekezo Haya Bajeti Kuu

 

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba leo, Jumatatu Machi 11.2024 amewasilisha mapendekezo ya mfumo na ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwenye kamati ya Bunge zima katika kikao kazi kilochofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni jijini Dodoma, ambapo serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 49.34 kwa mwaka 2024/25 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24 ya shilingi trilioni 44.39


Katika kikao kazi hicho kilochoongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, pia kimehudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mussa Azan Zungu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad