NAHITIMISHA MJADALA KATI YA CHAMA NA PACCOME
Hatukatai Chama Jana alikuwa kwenye kiwango chake kile kile cha siku zote hasa anapo kutana na timu za daraja la kati, ndio maana hata mzee SAID NTOMBOKIZA ANT BAYOOOOTIK leo pia alikuwa moto wa kuotea mbali tofauti na inavyo kuwa anapocheza na timu ngumu ambapo mara nyingi tunasikia lawama zikienda kwa SAIDI kila anapo gusa mpira.
Hivyo basi kucheza kwake vizuri Chama kusipelekee mkaanza porojo kwamba ni bora kuliko PACOME. Kwanza kabisa kwenye kundi la Yanga hakukuwa na timu sampuli ya Jwaneng hilo tuweke sawa.
PACOME ameziadhabu timu zote kwenye kundi. Ameifunga nje ndani Medeama bingwa wa Ghana..
Ameifunga Al Ahly bingwa wa Misri juzi katoa pasi ya Goli kwa bingwa wa Algeria. Pia mbali na kutoa pasi ya Goli, vile vile ni mchezaji aliye sumbua ndani ya dakika 90.
Sitaki kugusia mechi ile ya Goli tano, maana kila mtu aliona jinsi PACOME alivyo wafundisha mpira viungo wenu wakiongozwa na CHAMA picha na video zipo. Hivyo basi ili uwe mchezaji hatari kuliko mwenzako, pafomu vizuri kwa kila mechi iwe ngumu au nyepesi.
Chama hakuna alicho kifanya kwa Asec wala hakufanya chochote dhidi ya Wydad. Itoshe kusema huyu ni mchezaji wa mechi nyepesi, laiti hawa Jwaneng wangekutana na Yanga pengine leo PACOME angeondoka na mpira. Acheni kusifiana ujinga.
Nb/Chama alicho mzidi Pacomé ni umasikini na uzee tu.