Jeshi la Polisi limesema hakuna kampuni iliyopewa kibali cha kutengeneza namba za magari zilizoongezwa ukubwa maarufu kama (3D) bali zote zinatengenezwa kinyemela na kuwataka walioweka namba hizo waziondoe kwakuwa zinahatarisha usalama kutokana na na namba hizo kutosomeka vizuri wakati gari likiwa mbali au kwa pembeni.
Kwenye mahojiano maalum na @AyoTV_, Mkuu wa Elimu Kikosi cha Trafiki Tanzania, ACP Maiko Deleli amesema endapo namba hizo zisipodhibitiwa zitasababisha Watu kufanya uhalifu na kukimbia bila namba zao kujulikana “Hizi 3D ukiwa angle fulani ukaangalia pembeni hivi huwezi kuisoma kwasababu ya ujazo ila zile nyingine unasoma, hili imeanza kuleta tatizo kwetu, herufi pia zinakubaliana na inafanya hata Mtu akikuacha hatua tu 20 namba huwezi kuisoma lakini pia 3D zinaakisi mwanga wa jua ukipiga hauwezi kuisoma namba”
“Hakuna kampuni iliyopewa kazi ya kubandika 3D bali hii inafanywa kinyemela tu, hakuna Mtu aliyeruhusiwa kuweka 3D”
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetangaza siku 14 kuanzia March 4 2024 kwa Watumiaji wa Vyombo vya moto barabarani kuondoa namba za 3D, vimulimuli kwa magari yote yasiyoruhusiwa kuwekwa, namba zote zenye vibao vyeusi na wanaotumia namba za chasis, taa zozote pamoja na stika ambazo zimeongezwa kwa matakwa ya Wamiliki au Madereva,