Rais Museveni amteua mtoto wake kuwa kamanda mkuu wa jeshi



Rais Museveni amemteua mtoto wake wa kiume Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa kamanda mkuu wa jeshi, uteuzi huo hata hivyo umezua minong'ono huku wengi wakiamini kuwa Museveni anamsafishia njia mtoto huyo kuwa rais.

Muhoozi Kainerugaba anachukua nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbadi ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa biashara katika mabadiliko mapya ya baraza la mawaziri yaliyotangazwa jana jioni.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi, washauri wake wawili wa karibu pia wamepewa nyadhifa za uwaziri na kuchochea uvumi kwamba Rais Museveni anaunga mkono shughuli za kisiasa Muhoozi Kainerugaba.

Mtoto huyo wa kwanza wa rais amekuwa akifanya mikutano ya hadhara kote nchini, hatua ambayo inakwenda kinyume na sheria inayowazuia maafisa wa jeshi kujihusisha na siasa zenye kuegemea mrengo fulani.

Kainerugaba hata hivyo amejitetea kwa kueleza kuwa shughuli zake - ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa hivi karibuni wa kundi la uanaharakati la Patriotic League of Uganda- aliyesema kundi hilo linanuia kuhimiza kujenga uzalendo miongoni mwa Waganda

Museveni ambaye kwa mara ya kwanza alichukua madaraka kwa nguvu mnamo mwaka 1986, na kuchaguliwa mara sita, hajaeleza ni lini atakapostaafu.

Kiongozi huyo pia hana mpinzani ndani ya chama tawala cha NRM huku wengi wakiamini kuwa jeshi litakuwa na sauti katika kuchagua mrithi wake.

Kulingana na wachambuzi, washirika wa Kainerugaba wameteuliwa kimkakati kwenye nafasi za juu za idara ya usalama. Uganda itaanda uchaguzi mkuu ujao mwaka 2026.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad