Rais Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pongezi kwa Rais mteule wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili Machi 24, 2024.
“Nawasilisha pongezi zangu za dhati kwa mheshimiwa Bassirou Diomaye Faye, Rais mteule wa Jamhuri ya Senegal, kwa ushindi wako katika uchaguzi wa urais wa 2024 wa Senegal; na watu wa Senegal kwa uchaguzi wa amani. Natarajia kuendelea kufanya kazi pamoja ili kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Senegal,”ameandika Rais Samia katika mitandao yake ya kijamii.
Faye anaingia madarakani baada ya kumshinda mpinzani wake mkuu kutoka muungano wa chama tawala, Amadou Ba, ambaye alikuwa Rais wa Senegal.