Rapa Meek Mill(36) akana kwa nguvu zote kuwa shoga, ni baada ya kuhusishwa katika waraka wa kesi mpya ya mahakama aliyofunguliwa Diddy(54) kwa kudaiwa kumnyanyasa kingono producer wake wa kiume
Wiki hii producer Rodney Jones aliyehusika kutengeneza nyimbo za "The Love Album" ya Diddy iliyotoka 2023, ameibuka kumfungulia kesi Diddy kwa kumtuhumu kumnyanyasa kingono ikiwemo kumgusa kwa mpalange bila ridhaa yake
Producer amesema katika kumshawishi, Diddy alimwambia tayari alishalala na watu kadhaa maarufu wengine si wasanii ila wana majina makubwa. Jina la Meek Mill halikutajwa moja kwa moja katika waraka wa mahakama ila producer amedokeza kwa kusema Diddy alishamwambia kalala hadi na msanii wa hip hop anayetokea jimbo la Philadelphia ambaye ni ex wa Nicki Minaj
Kidokezo hicho moja kwa moja kikapelekea watu wajue ni Meek Mill hivyo watu kumuibukia mtandaoni kuanza kumpopoa na kusababisha rapa huyo kuachia jumbe fupi mfululizo kukakana kupitia mtandao wa X zamani Twitter, Meek amesema yeye anavutiwa na wanawake si vinginevyo hivyo yeye sio shoga wala hajawahi kuwa na Diddy kimwili kama inavyodaiwa
Hata hivyo, producer ameweka wazi kuwa yeye anavutiwa na wanawake sio wanaume hivyo kamkatalia Diddy adhma yake. Ila katika waraka wa mahakama ameambatanisha screenshots mbalimbali anazodai ni za ushahidi ukiwemo wa videos kuhusu Diddy kwasababu pia amedai Diddy kuna wakati alikuwa anajisahau anachukua simu ya producer na kuanza kujirekodi mwenyewe vidoes mbalimbali na kusahau kufuta. Pia ameeleza kupata ushahidi wa vidoes kadhaa toka nyumbani kwa Diddy huku akisangaa na kuhoji kwanini Diddy hachukuliwi hatua kwani yupo juu ya sheria !
Katika waraka husika wa kurasa 75, producer Rodney ameeleza mambo mengi sana kumhusu Diddy ikiwemo kulazimisha mtu kutumia madawa ya kulevya, kurekodi watu bila ridhaa yao nyumbani kwake kwa kamera za siri katika house parties wakiwa faragha, amemhusisha Diddy na ngono za watoto, kutumia silaha za moto ovyo kinyume na sheria ikiwemo mtu kupigwa risasi kwenye viunga vya jengo lake
Pia watoto wa wawili wa Diddy wametajwa katika waraka husika kwenye mambo yasiyokubalika sheria ingawa sio ya ushoga, washirika wa Diddy pia wametajwa