Sababu ya Beki Dickson Job Kuachwa Katika Kikosi Kipya Cha Taifa Stars Hizi Hapa


Sababu ya Beki Dickson Job Kuachwa Katika Kikosi Kipya Cha Taifa Stars Hizi Hapa

Sababu kubwa na ya msingi ya kuachwa Dick Job ni utovu wa nidhamu na kukosa uzalendo kwa kitendo cha kukataa kucheza mechi dhidi ya Congo DR ambayo ilikuwa muhimu kwa Taifa Stars mchezo uliochezwa pale Korogho Ivory Coast.

“Kocha Morocco aliyekuwa anakaimu ukocha wa Stars baada ya Amrouche kusimamishwa na CAF, alimpanga Job nafasi ya beki wa pembeni kulia (namba 2), kisha akaita kikosi kufanya nacho kikao kazi kabla ya mechi na kuelekeza mbinu za kuikabili DRC kwenye mchezo huo, baada ya kumaliza ndipo Job alinyoosha kidole akasema yeye hayuko tayari kucheza namba 2.

“Ikabidi kocha ambadilishe na nafasi yake kupewa Lusajo Mwaikenda wa Azam ambaye alipambania Taifa mpaka mwisho. Inaelezwa nahodha wa Stars MBWANA Samatta aliongea na kocha kwamba angeongea na Job ili acheze lakini kocha akamwambia muache usimlazimishe. Mechi iliisha kwa sare ya 0-0.” — @jemedarisaid ✍🏾

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad