Serikali: Waziri Ndumbaro alikuwa anatania suala la "Passport" kwa Mkapa

 

Serikali: Waziri Ndumbaro alikuwa anatania suala la "Passport" kwa Mkapa

Waziri Ndumbaro alikuwa anatania


Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi ametoa ufafanuzi kuhusu kauli ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro kwamba Shabiki atakayekwenda uwanjani kutazama mechi za Kimataifa za Simba na Yanga anapaswa kuvaa jezi za Simba au Yanga kinyume na hapo atalazimika kuwa na passport ya Nchi ambayo klabu anayoishangilia inatokea au vinginevyo hatoruhusiwa kuingia uwanjani.


Msemaji Mkuu katika ufafanuzi wake leo amesema Waziri alikuwa anahamasisha tu uzalendo wa Timu na hakumaanisha kuwa kweli Watu watazuiliwa kisa pasport.


“Alichozungumza Mh. Waziri (Dkt.Ndumbaro) alikuwa anahamasisha uzalendo wa Timu zetu na katika lugha zetu za michezo Waandishi wa Michezo tunafahamu, Mimi niliwahi kuwa wakati fulani Mwandishi wa Michezo na niliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) sisi tukizungumza 80% ni utani, 20% tunazungumza vitu vimekaa vimenyooka”


“Ukizungumza habari zinazohusisha Simba na Yanga, ukang’ang’ana kuzungumza kitu kama kilivyoandikwa mahali fulani hivi inafika mahali unawachosha Watu, hizi ni Timu zinazopenda utani ni Timu zinazopokea ujumbe wakati mwingine kwa lugha rahisi, si kweli kwamba Mh. Waziri alimaanisha pale itakaguliwa pasport, anayejua pasport halali na isiyo halali ni Idara ya Uhamiaji, hakusema Idara ya Uhamiaji itaenda uwanjani pale”


“Kwahiyo katika ushabiki huohuo wa mpira Watu wamelifanya jambo hili la mzaha wamelikuza mpaka Mamelodi wamesikia wameingia uoga, na wameandikiwa na TFF lakini Mimi niwasihi Watanzania tuwe Wazalendo na tutarajie Mamelodi watafungwa na Al Ahly nao watafungwa magoli ya kutosha”


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad