Upande wa pili wa kauli ya Mwekezaji
Kama tajiri amemaanisha kununua hisa ambazo ni 49% kuna vitu vya kujiuliza pia na hapa.
1 . Mfumo wa mabadiliko ambao ndani yake ndio kuna hayo mauziano ya hisa na kutafsirika kama uendeshaji wa timu kisasa huo mfumo wa mabadiliko umekamilika ? Jibu ni Hapana
2. Kama bado , hizo hisa 49 % unazinunua kwa utaratibu upi ?
Kwa faida tu .
January 18 Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria wa Simba, Wakili Hussein Kitta alisema maboresho ya rasimu ya Katiba ya Simba yaliyofanywa kama wanachama watapitisha, basi mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo utafanikiwa ndani ya muda mfupi , maana yake ni kwamba mchakato wa mabadiliko haujakamilika.
Nukuu 🎤
“Maboresho ambayo tumeyafanya na vitu ambavyo tulivyoviboresha kwenye rasimu ya Katiba ikitokea wanachama wameipitisha, mchakato wa mabadiliko utafanikiwa ndani ya muda mfupi tofauti na ambavyo mchakato huo wa mabadiliko ulikwama kwa zaidi ya miaka mitano.”
Tarehe 18 hiyo hiyo Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa nchini Ivory Coast, alitolea ufafanuzi mchakato wa katiba mpya ya Simba na alisisitiza sheria na kanuni ziheshimiwe akaongeza kwa kusema wizara haijapitisha katiba ya Simba.
Nukuu 🎤
“Wizara haijapitisha katiba ya Simba,katiba ya Simba ilikuwa na mapungufu na ilikiuka sheria za ushindani wa haki ,RITA na BMT ! maelekezo ambayo wamepewa Simba ni kwamba lazima waheshimu sheria”
Tafsiri yake sasa ni kwamba kama katiba bado maana yake mchakato wa mabadiliko pia bado ,kama mchakato wa mabadiliko bado mauziano ya hisa pia bado kama hisa tu mauziano bado Tajiri ameuziwaje hii timu_____?
Hizi kauli ni za January 2024 , Tajiri anasema ameinunua hii timu mwaka wa tano sasa