Shekh Abdulrazak Akana Kwamba Alikuwa Akilelewa na Diva



Abdulrazak amekana kwamba alikuwa akilelewa na Diva. Akihojiwa na Rickmedia , Abdul amesema kuna mambo Diva alikuwa akiyafanya kwake kwa mapenzi yake mwenyewe

Vilevile, Abdul ameweka wazi kuwa yeye kwa mwezi hana uwezo wa kulipia kodi ya shilingi milioni 5 katika nyumba aliyokuwa akiishi mtangazaji huyo maarufu. Abdul amesema hawezi kupoteza milioni 5 kwa kodi tu wakati ana mambo mengine ya muhimu ya kufanya

Baada ya hapo, Diva ameona post husika na kumkoromea Abdul aache maneno mengi bali ampe talaka yake ambayo amekuwa akiidai kwa muda sasa ila Abdul hataki kutoa talaka licha ya Diva kusema kachoka kuumizwa katika ndoa kwa mambo mengi anayofanyiwa na Abdul ukiwemo usaliti wa mara kwa mara

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad