Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetuma barua katika Shirikisho la Soka Barani Africa (CAF), kulihakikishia kuwa mechi ya Yanga SC dhidi ya Mamelodi Sundowns itachezwa kwa kanuni na taratibu zilizowekwa na namna ya kuingia uwanjani na kigezo sio Passport.
Hatua hiyo imefikia mara baada ya siku chache Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Damas Ndumbaro kuwataka mashabiki kuvaa jezi za klabu za Tanzania hasa kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Mamelodi, huku Simba wakicheza dhidi ya Al Ahly.
Katika barua hiyo, TFF wameiambia CAF kuwa, utaratibu wa michezo hiyo utafuatwa kama kawaida na suala la mashabiki kuingia passport sio kigezo kwa sababu michezo hiyo haipo chini ya Idara ya Uhamiaji
.
.