Tunda Amvua Nguo Whozu "We Bogus Nilidhani Utakuwa Mjanja Baada ya Kutoka na Wema"



Tunda amnyumbua na kumtwanga Whozu kwa kumfuatafuata baada ya kuachwa na Wema Sepetu

Tunda ameipost video iliyosambaa Whozu akimuongelea katika mahojiano aliyofanya, kisha kumlipua baba mtoto wake huyo ambaye waliachana muda sasa kila mmoja akawa na mahusiano mengine

"Msikilizeni kwa makini huyu b*gus...yaani aniseme mimi halafu mimi kumsema anapanic nini?. Uongo nini hapo unanipenda unahangaika na mimi sana mnoo yaani wewe hata upate mwanamke wa aina gani huwezi ku-move on kwangu huwezi yaani

Nilitegemea ume-date mtu mkubwa zaidi yangu(Wema Sepetu) maarufu zaidi itakuwa afadhali umezoea utaishi kinyamwezi lakini wapiiii !! ndio kwanza ak1li yako iko nyuma tu ....tulia nakuonya kwa mara ya mwisho

Acha kusumbua marafiki zangu acha mara moja ulianza na kina Davto kipindi cha nyuma kuwafuatafuata mpaka nikaamua nikuachie sasa hivi nimepata rafiki mwingine kutwa kumganda kumsumbua simu kumfuatafuata nyumbani achana na watu wangu kwani wanawake wako hawana marafiki ????

Halafu ukiambia unanipenda mtandaoni unalialia" - amesema Tunda ambaye ana mtoto mmoja aliyezaa na Whozu

Whozu aliripotiwa kumpiga Wema Sepetu hali ambayo Wema mwenyewe hakuipenda na kumuacha huku familia ya Wema muda mrefu hasa Mama Wema kuonesha wazi kutoridhishwa mwanae kuwa katika mahusiano na mwanamuziki huyo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad