Uongozi wa WCB Wasafi Imekanusha Mlinzi wao Kumshambulia Mwandishi



Uongozi wa WCB Wasafi imekanusha madai ya shambulizi dhidi ya mwandishi wa habari na inasisitiza kwamba mlinzi wa Diamond Platnumz alifuata sheria katika kumlinda mwandishi.

Wanathibitisha kuwa hakukuwa na shambulizi kama ilivyodaiwa na wanatoa wito kwa vyombo vya habari kufuata sheria na kuepuka kutengeneza habari za uongo. Pia, wameishukuru vyombo vya habari kwa ushirikiano wao na wanaahidi kuendelea kufanya kazi nao kwa karibu.

"Menejimenti ya Lebo ya WCB Wasafi inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma juu ya taarifa zinazosambazwa kuhusiana na mlinzi binafsi wa Msanii Nasibu Abdul Juma Issaack almaarufu kama Diamond Platnumz. Mlinzi wa msanii anahusishwa na kumshambulia mwandishi wa Bongo Star Media TV baada ya Tamasha Usiku wa tarehe 24/02/2024 kisiwani Zanzibar".

"Menejimenti inapenda kuujulisha umma ya kuwa taarifa hizo sio za kweli na zenye mlengo wa kupotosha na kupandikiza chuki. Ukweli wa jambo hili ni kwamba, mwandishi huyo alivuka mipaka ya sheria za kupata habari kwakujaribu kulazimisha kwenda kuwarekodi wasanii Diamond na Zuchu katika eneo la hoteli ambalo waandishi wa habari hawaruhusiwi kuingia bali kwa wakazi wa hoteli hiyo pekee. Mlinzi tajwa na wenzie walitumia njia zinazoheshimu na kulinda haki za waandishi wa habari katika kumzuia."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad