Ameandika Haya:
"Haya mambo yanaendelea kwenye Ligi namba 5 Afrika ?
Kama ilivyo kwa wafuatiliaji wengine wa mpira wa miguu huku mtandaoni ,mimi pia nimekutana na hii clip siku ya jana .
Binafsi sijashangaa sana hii kauli ya Prince Dube kwa sababu sio mpya kabisa hasa kwa wadau ambao wapo ndani ya mpira wetu.
Lakini nimeichukua hii nikawaza kwa ukubwa ambao ligi yetu inao huko nje , sasa hivi kwenye Ligi 10 bora Afrika NBCPL pia ipo tena namba tano.
Dube ameiongea hii huwenda ni kwa sababu ameondoka lakini ukweli ni kwamba hata wachezaji ambao wapo ndani ya klabu zingine hii mizengwe wanaifahamu
Maana yake kama picha ndio hii huko kambini na kwenye dressing room,itatuchukua muda mrefu sana kuona kuna timu nyingine inasimama na kuwa bingwa mbele ya Simba na Yanga.
Kwenye picha ya uwekezaji ,hii clip kama inamfikia mmiliki wa timu anambiwa kuwa amewaajiri washindani ambao wanarudisha nyuma ushindani hii ni mbaya sana .
Kuwa muajiriwa wa taasisi fulani na unamapenzi na taasisi nyingine hii ipo lakini sio sawa kuingiza mapenzi yako kwenye utendaji kiasi cha kuwarudisha nyuma waliokuamini na wanaokupa ugaliTunapambana kupunguza changamoto ya ajira mtaani kupitia michezo itakuwaje tajiri akiamua kuachana na biashara ambayo anaona haiingizi faida kwa sababu ya watu wachache tu wanaoshindwa kuthamini juhudi za wawekezaji vijana wangapi watarudi mtaani ? Je Matajiri wangapi wanaowaza kuingia kwenye hii biashara watavunjika moyo ?
Hii ni wake up call" Shaffih Dauda