Walioleta Nchini Internet ya Starlink Wakamatwa na polisi

Walioleta Nchini Internet ya Starlink Wakamatwa na polisi
 Internet ya Starlink 

Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana na matumizi ya makosa ya kimtandao limewakamata Claudian Makaranga (28) mkazi Kawe na Hongliang Yang (35) Mchina, mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kuingiza vifaa vya mawasiliano.

Vifaa hivyo vya mawasiliano ya ya intaneti vyenye jina la STARLINK KIT/DEVICE vimeingizwa hapa nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria.


Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum SACP Jumanne Muliro anasema Watuhumiwa hao wamekuwa wakijitangaza kuuza vifaa na kutoa huduma ya internet nchini kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram kwa akaunti yenye jina la STARLINK.


Baadhi ya vifaa vilivyoingizwa nchini imebanika vilishauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kitendo ambacho ni kosa na kinyume na sheria kwani havijaidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad