Wauaji wa Shambulio Urusi Wafikishwa Mahakamani



Vijana wanne waliohusika kwenye shambulio lililoua watu zaidi ya 130 nchini Urusi katika eneo la Crocus City Hall, wamefikishwa Mahakamani wakiwa na majeraha.

Majeraha hayo yametokana na nguvu iliotumika ili kufanikisha kuwakamata. Washtakiwa hao wote wametambuliwa kwa majina ambayo ni Saidakrami Murodali (30), Dalerdzhon Mirzoyev (32), Shamsidin Fariduni (25) na Muhammadsobir Fayzov mwenye miaka 19.

Washtakiwa wote wamekiri kuhusika na mauaji hayo, hivyo kesi imeahirishwa na wataendelea kubaki mahabusu hadi watakaporejeshwa Mahakamani Mei 22, 2024.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad