Waziri Makamba Akanusha Uwepo wa Noti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki


Makamba

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (@jmakamba) amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni usiku huu zikidai kwamba, Jumuiya ya Afrika Mashariki imetambulisha Noti yake ambayo imepewa jina la SHEAFRA.

Kupitia ukurasa wake wa X, Makamba ameandika “Hizi taarifa sio za kweli. Taratibu na vigezo, vya kiuchumi na kitaasisi, vya kufikiwa kwa Umoja wa Fedha (Monetary Union) na Sarafu Moja (Single Currency) kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki bado kukamilika. Mapendekezo mapya ni 3031. Ukurasa rasmi wa Jumuiya ni ‘Jumuiya’ “ ameandika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad