Waziri Silaa Aingilia Kati Mgogoro wa Eneo la Jengo la Ghorofa Kariakoo Lililowekwa Wakfu



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa ameingilia kati mgogoro wa eneo la jengo la ghorofa lilipo Kariakoo jijini Dar es salaam ambalo sehemu ya jengo hilo lilitolewa Waqfu na marehemu Sheikh Mohamed Ardini ambaye aliacha usia.

Waziri Silaa alifika eneo hilo ambalo limekuwa na ugomvi mkubwa wa ndugu ambao ni watoto wa marehemu Ardini waliogawanyika katika pande mbili zinazokinzana kuhusu usia wa kuwekwa Waqfu eneo la Madrasa katika jengo hilo.

Aidha, baada ya kusikilizwa kwa pande mbili za ndugu ambao ni watoto wa marehem Mzee Ardini Waziri Silaa aliamuru kurejeshwa kwa Madrasa ambayo ilikuwa ndio usia wa marehem.

Awali, ndugu wawili wanao pingana na wenzao waliamua kuhamishwa kwa madrasa hiyo nje ya eneo hilo la Kariakoo na kumuuzia mtu mwingine sehemu ya jengo hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad