Waziri "Watakao Vaa Jezi za Mamelod na Al Ahly Waje na Passport zao Uwanjani



Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani, Kimeendelea na Operesheni ya kutoa elimu na kuwakamata wale wote wanaoendelea kuvunja sheria za usalama barabarani huku Jeshi hilo likiwapongeza wale wote waliotii agizo la Serikali la kuondoa namba ambazo hazijathibitishwa na Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS).

Akiwa katika Operesheni hiyo leo Machi 19, 2024 Mkoani Arusha Mkuu wa Operesheni za kikosi cha Usalama barabarani Nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP, Nasoro Sisiwayah amesema kikosi hicho kinaendelea kuwakamata wale wote waliokaidi agizo la kuondoa namba zenye ujazo 3D na ving’ora.

ACP Sisiwayah ameongeza kuwa Operesheni hiyo imelenga pia kukamata madeni ya wale wote waliofanya makosa barabarani na kupigwa faini ambapo amebainisha kuwa zoezi hilo linaendela nchi nzima huku akiwaomba watumiaji wa vyombo vya moto ambao wanadaiwa kuhakikisha wanalipa madeni yao kwa wakati.

Aidha amesema kuwa operesheni hiyo pia imehusisha kuwakamata wale wote wanaoendesha mwendo kasi vyombo vya moto ambapo amebainisha kuwa uchunguzi wa Jeshi hilo unapofanyika umebaini kuwa chanzo cha ajali nyingi ni mwendo kasi hivyo nao watakamatwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad