Yanga na Azam Hawajawahi Kutupa Game Mbovu, Sema Yanga Wanamuitaji Aucho sana


Yanga na Azam hawajawahi kutupa game mbovu , wanatoa mchezo bora sana : High Intensity , Ufundi wa hali ya juu na magoli utashuudia .

Yanga kama kawaida yao 4-2-3-1 , Sure na Muda kwenye viungo wawili wa chini . Yanga wakiwa na mpira hawakubadilisha “Script yao” Muda anasogea juu sawa na Pacome / Mzize , Maxi na Aziz Ki ambao walikuwa wanacheza kwenye mstari mdogo sana wa kiungo cha Azam . Kivipi ?

Azam walizuia wakiwa chini sana 5-3-2 na walikuwa karibu karibu sana pia hawakuacha nafasi kwenye maeneo matatu (Ulinzi , Kiungo na Ushambuliaji) waliwalazimisha Yanga kuunda mashambulizi kupitia pembeni ya uwanja , then walinzi wa katikati walicheza mipira mingi ya juu … Yanga walipata nafasi za wazi ni wao tu . UFANISI MDOGO .

Yanga wasipokuwa na mpira walikuwa wazi sana , hasa kwenye eneo la kiungo (Muda Aziz na Maxi walikuwa mbali sana na Sure …. Azam walitengeneza “Overload” walipata nafasi kubwa sana : utulivu , umakini kwenye maamuzi yao ndio hayakuwa sahihi . Yanga baada ya kuona Azam wapo chini walicheza na wachezaji wengi wenye “Attacking Minded” lakini bado walikosa nafasi eneo la mbele .

NOTE:

Yanga wanamuhitaji “Aucho” kwenye kiungo aisee wapo wazi sana …. Azam hawakuhitaji kazi kubwa kuivuka kiungo cha Yanga .

Feisal “Goli la 13” Anawapa Azam Alama 3 …. Yahya Zaid Azam wakianza “Build Up” 🔥 …. Kipre Jr Kasi , Ufundi ✅

Job amecheza vizuri sana : Sure akiwa na mpira 🔥

FT: Azam 2-1 Yanga

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad