Yanga Yaendelea Kuwa Mateja wa Al Ahly, Wachapwa Cairo

Yanga Yaendelea Kuwa Mateja wa Al Ahly, Wachapwa Cairo


Timu ya Yanga imekamilisha mechi zake za Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa 1-0 na wenyeji, Al Ahly usiku wa Jana Machi 1 Uwanja wa Venue Cairo International Jijini Cairo nchini Misri.


Bao pekee la mabingwa hao watetezi limefungwa na kiungo mkongwe Mmisri Hussein El Shahat dakika ya 46 akimalizia pasi ya beki Mtunisia, Ali Maâloul.


Mechi nyingine ya Kundi D leo wenyeji, CR Belouizdad wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Medeama SC ya Ghana, mabao ya Abdelraouf Benguit dakika ya 27, Leonel Wamba dakika ya 42 na Lamin Jallow dakika ya 84 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers.


Al Ahly inamaliza kileleni mwa Kundi D kwa pointi zake 12, ikifuatiwa na Yanga pointi nane na zote zinafuzu Robó Fainali, wakati CR Belouizdad iliyomaliza na pointi nane pia ikizidiwa wastani wa mabao na Yanga na Medeama SC iliyomaliza na pointi nne zote safari yao inaishia hapa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad