Imeelezwa Februari 24, 2024, Zuchu wakati akitumbuiza katika usiku wa Fullmoon Kendwa inadaiwa aliimba nyimbo, kutoa matamshi na kuonyesha ishara mbaya ambazo ni kinyume na Maadili ya Zanzibari
Katibu Mtendaji wa Baraza, Omar Abdalla Adam amesema pia Zuchu ametakiwa kulipa faini ya Tsh. 1,000,000 kwa Baraza na aandike barua ya kuomba radhi na kuthibitisha kwamba hatafanya kosa hilo ndani ya kipindi alichofungiwa, iwapo hatafanya hivyo zuio lake litaendelea kwa muda usiojulikana