Ahmed Ally: Serikali Kulipia Mashabiki wa Yanga sio Jambo Jema

 

Ahmed Ally: Serikali Kulipia Mashabiki wa Yanga sio Jambo Jema

Anaandika Meneja wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally kupitia Instagram yake; --------- Baadhi ya Mashabiki wa Simba waliojilipia nauli zao kusafiri kwenda kuipa support timu yao Nchini Misri


Kila shabiki amejilipia Dola 1200 sawa na Milioni 3,126,000


Hili swala la Serikali kusafirisha Mashabiki nitatoa maoni yangu nikimalizana na Al Ahly, Sasa hivi akili inawaza namna ya kufuzu Nusu Fainali, Ila msimamo wangu ni kwamba si jambo jema hata kidogo


Kwa Mashabiki mpira ni starehe hivyo Serikali haiwezi kugharamia watu kwenda kustarehe.


Tena bora ingekua imetoa usafiri tu. Lakini wametoa Posho Dola 500 kila kichwa sawa na Milioni 1,200,000 kwa ufupi hawa Mashabiki wamenuniliwa na wanalipwa kuishangilia timu yao


Na hao sio Mashabiki wa kawaida ni Machawa wanaotetea maslahi ya viongozi wao yaani Serikali imelipia Machawa wa watu


Kuwalipia nauli sio kuwapenda ni kufuga tatizo ambalo baadae hatutaweza kulitatua


Leo unalipia mashabiki wa klabu, kesho Ali Kiba ataiomba Serikali iwagharamie mashabiki wake kwenda Marekani kufanya show utamnyima??


Twaha Kiduku ataomba aende kupigana Uingereza na mashabiki wake utamnyima??


Halafu nyie Nyuma Mwiko acheni kuzuga huwezi kulipia nauli watu 48 ukajidai eti unawapenda mashabiki zenu, Wakati kwenye mechi yenu juzi Mashabiki wameumia, wamepigwa mabomu ya machozi, watu wamepata vilema, na hamjasema chochote halafu uje uzuge eti unawapenda watu wenu


Ndugu zangu wana Simba hili swala lisiwatie unyonge na wala Serikali yetu haina nia ya kufanya ubaguzi


Sisi tuendelee na utamaduni wetu kujisimamia tukipata msaada tutachukua lakini katu tusilemae kusubiri dezo


We are Simba Sisi ni Wakubwa, Sisi ni Wafalme, Sisi tuna hadhi kubwa


Lets focus na mechi yetu ya Ijumaa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad