Tangu msimu unaanza mimi ni miongoni mwa watu ambao walikutana na upinzani mkubwa sana kwa sababu nilikuwa siamini kama Simba wanaweza kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu kwa sababu ya mabadiliko wanayoendelea kuyafanya kwenye timu yao.
Nilikuwa naamini kuwa wataweza kutetea nafasi ambayo walimaliza msimu uliopita lakini wakiendelea kuimarika. Simba wao waliendelea kuamini wapo tayari kuchukua ubingwa msimu huu.
Simba walianza kutuonesha kuwa hawapo tayari kutwaa ubingwa wa Ligi msimu huu tangu kwenye mechi za Ngao ya Jamii. Walifanikiwa kuchukua ubingwa wa Ngao ya Jamii lakini hawakuonesha kiwango kizuri uwanjani.
Kama ubingwa ungekuwa unatolewa kulingana na kiwango cha timu uwanjani, Simba ingekuwa timu ya mwisho [4]. Yanga wangekuwa namba moja, Azam wangefuata, Singida Fountain Gate halafu Simba wangemaliza.
Simba kuwa bingwa wa Ngao ya Jamii kulificha mapungufu yao mengi sana na watu wakajificha humo kwamba zimeshiriki timu nne bora za msimu uliopita lakini wao ndio mabingwa.
- Amri Kiemba, Mchambuzi Clouds Media Group.