Benchikha: Matatizo yameniondoa Simba SC

 

Benchikha: Matatizo yameniondoa Simba SC

Kocha kutoka nchini Algeria Abdelhak Benchikha ametoa sababu za kuondoka Simba SC, baada ya Uongozi wa klabu hiyo kuthibitisha kuvunja mkataba na kocha huyo jana Jumapili (Aprili 28).


Benchikha alijiunga na Simba SC Novemba mwaka 2023, baada ya kuachana na Klabu ya USMA ya nchini kwao Algeria na alipewa jukumu la kuivusha klabu hiyo ya Msimbazi kutoka Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na kuipeleka Nusu Fainali.


Kabla ya kuondoka nchini Tanzania usiku wa kuamkia leo Jumatatu (Aprili 29), Kocha Benchikha amesema sababu kubwa ya kulazimika kusitisha mkataba wake na Simba SC ni matatizo ya kifamilia yanayomkabili kwa sasa.


Amesema alitamani kuendelea kufanya kazi na klabu hiyo, lakini amelazimika kuondoka huku akihidi huenda kuna siku akarejea Msimbazi kufanya kazi kwa mara nyingine, na kama itashindikana bado ataendelea kushirikiana na viongozi na wachezaji wa klabu hiyo.


“Malengo yangu makubwa yalikuwa ni kwenda Nusu Fainali ya Klabu Bingwa na kufika Fainali na hata kutwaa Ubingwa, lakini kwa bahati mbaya haikuwa bahati kwetu, ninaamini ilikuwa ni mipango ya Mungu,”


“Ninakiri wazi kuwa Al Ahly ni klabu kubwa, licha ya kutufunga katika hatua ya Robo Fainali, lakini nilidhamiria kushinda mchezo ule, kwa bahati mbaya sikufanikiwa.”


“Suala la kuondoka kwangu halina tatizo lolote na Uongozi wa klabu ya Simba SC, ninataka mashabiki wafahamu kuwa nina tatizo la kifamilia, niweke wazi mke wangu ana tatizo la kiafya ambalo limesababisha kusitisha mkataba wangu na Klabu hii ambayo ninakiri ninaipenda sana.”


“Tatizo hili la kiafya la mke wangu lilipeleka akili yangu kushindwa kutulia, kwa hiyo niliona kuna haja ya kuongea na Uongozo wangu ili kupata wasaa wa kurudi nyumbani kushirikiana na familia yangu kumuuga mke wangu.”


“Nilitamani kulitatua tatizo la mke wangu nikiwa hapa Tanzania, lakini imeshindikana, Uongozi wa Simba SC ulinionesha ushirikiano mkubwa katika hili, lakini bado nikaona kuna haja ya kurudi nyumbani ili niwe karibu na mke wangu.”


“Nikiwa hapa Tanzania nimeshangazwa sana na upendo wa Mashabiki wa klabu ya Simba SC, kumbuka sikiwahi kufanya kazi hapa lakini niliishi kama mwenyeji, kwa maana kila mahala nilipopita niliona upendo kutoka kwao, na hili ndilo linalofanya niseme kuwa ipo siku nitarudi kufanya kazi tena hapa.


“Hata ikitokea sitarudi ninawahakikishia wanasimba kuwa timu hii ipo moyoni mwangu, nitaendelea kupambania hata nikiwa nyumbani, kwa kuonesha ushirikiano wowote utakaohitajika kutoka kwa viongozi ama wachezaji.” Amesema Benchikha

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad