Bureau de Change' Zilizofungwa Nchini Kufunguliwa

 

Bureau de Change' Zilizofungwa Nchini Kufunguliwa

Serikali ipo mbioni kufungulia maduka ya kubadilisha fedha nchini (Bureau de change), ambayo yalifungiwa mwaka 2019 kutokana na tuhuma za utakatishaji fedha, huku wabunge wakitaka maduka yasiyo na hatia yalipwe fidia. - Akizungumza leo Aprili 2, 2024 Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan haipo tayari kuona rasilimali na fedha za mtu yeyote zilizochukuliwa zimebaki serikalini. - Chande alikua akijibu swali la Mbunge wa Chumbuni, Ussi Salum Pondeza aliyehoji sababu zilizosababisha maduka ya kubadilisha fedha kuondolewa katika biashara na wananchi wengi kupoteza ajira zao. - Chande amesema serikali itayafungulia maduka hayo muda wowote kuanzia sasa na kurudishiwa mali na fedha zao zote zilizopokwa na serikali katika operesheni iliyofanyika mwaka 2016.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad