Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi , amesema katika ziara yake ya siku 10 hadi kufikia sasa ametembelea mikoa sita na Nyanda za juu kusini ambapo kote alipopita amethibitishiwa na wanachama wa CCM kuwa wanataka Mwenyekiti wa Chama Taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, apewe miaka mitano mingine ya kuliongoza Taifa kutokana na kile wanachoendelea kukiona cha kufanyika kwa kazi kubwa na nzuri kila kona ya Nchi katika kuleta maendeleo kwa nchi na wanachi kwa ujumla.
Akizungumza kwenye mkutano ulioshirikisha Mabalozi wa mashina, viongozi mbalimbali wa chama na serikali, viongozi wa dini, taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali, wazee, machifu na wadau mbalimbali wa maendeleo, Balozi Dkt. Nchimbi amesema wanachoanua wanachama wa CCM ndicho kitakachotokelezwa kwasababu hakuna enek la nchi ambalo halijaguswa kimaendeleo na ndiyo sababu ya wababchama kufikia uamizi huo.
Aidha, Dkt. Nchimbi ametoa wito kwa wanachama wa CCM wa kuwatala kuendeleza umoja na mshimano kwasababu chama kina wajibu wa kuwatumikia Watanzania.
"Tukiwa na mshikamano nchi itashikamana, kama tukiwa na mafarakano na nchi itafarakana. Kila mwana CCM ajiulize anatoa mchango gani katika nchi yake ?"
"Kila mwana CCM ajiepushe kuwa chatu mbaya ndani ya chama na tujiepushe kwa kutimiza wajibu wetu. CCM lazima iendeee kuwa kimbiio la Watanzania."
"Kiongozi wa kweli hamdharau Mtanzania mwenzake bali ana wajibu wa kumpenda kila mtu, Chama hiki siyo viongozi ni chama cha wananchi"
Alisema Balozi Dkt. Nchimbi