“Ilichukua dakika nne tu Simba kuruhusu bao ambalo hakuna aliyejua lingebakia kuwa la pekee la mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mechi nyingine tatu zilizobakia kwenda suluhu ya bila kufungana wikiendi iliyopita.
.
Ndio, haikushangaza sana. Imekuwa kawaida ya Simba kuruhusu mabao. Simba sio ngumu kufungika. Kama wiki chache tu zilizopita ilimruhusu Samson Mbangula kufunga mabao mawili pale Morogoro basi ingekuwa ngumu kuwazuia Al Ahly wasipate bao Temeke.Ndicho kilichotokea.” — Edo Kumwembe.