EDO Kumwembe : Ni Muda wa Timu ya Simba Kujitafakari


Na sasa ni muda wa Simba kujitafakari. Wanatoka wapi na wanakwenda wapi? Yanga aliingia fainali za Shirikisho msimu uliopita na msimu huu ilibakia kidogo waende nusu fainali za Ligi ya mabingwa. Wana timu bora ambayo ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya ndani msimu huu na ina viongozi vijana ambao wanakwenda kasi.

Simba waige hili. Kutolewa pamoja na Yanga kusiwe faraja kwa Simba, bali waangalie mfumo wao wa kuingiza wachezaji klabuni. Simba inapaswa kurudi kule kwenye njia yake ambayo waliitumia hadi wakaweza kuongoza kundi lililokuwa na timu kali za kina Al Ahly na AS Vita. Kwa sasa unaona wazi kwamba makali yale hayapo na bahati mbaya kuna viongozi ndani ya Simba wanaona kama vile Yanga wanabahatisha.

Fitina za mpira katika Afrika zipo lakini unahitaji kuwa na timu bora. Ubora haujifichi uwanjani. Yanga walikuwa na kina David Molinga wakaishia kulalamika kwamba TFF walikuwa wanaibeba Simba. Sasa hivi wamekuwa na timu bora wamekaa kimya wakati uongozi wa TFF umeendelea kuwa ule ule tu.

Tusubiri kuona nini kitaendelea kuanzia sasa mpaka mwisho wa msimu na kisha katika dirisha la usajili. Kuna kitu lazima kibadilike kabla lawama hazijaanza kumshukia kocha Abdelhak Benchikha. Anaonekana kuwa na rekodi nzuri katika timu alizotoka lakini ni wazi kwamba alikuwa anasaidiwa pia na ubora wa wachezaji.” — Edo Kumwembe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad