DODOMA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Saidi Jafo amesema hoja ya kutaka kurejesha utaratibu wa Watu wa #TanzaniaBara kuingia #Zanzibar kwa Pasipoti ni kurudisha nyuma Muungano
Amesema “Kaka yangu pale alipozungumza kwamba, kwanini Watu wasiingie na Pasipoti Zanzibar, nikasema aah! Kaka wazo zuri lakini unataka kuturudisha nyuma. Serikali ya Awamu ya Pili chini ya hayati Mzee Mwinyi wakati kule Serikali iliyokuwa chini ya Rais Dkt. Salmin Amour, kipindi kile walikuwa wanajadili jambo hili lilitoka kipindi hicho likaonekana linaleta usumbufu.”
Amesema hayo akimjibu Mbunge wa Konde, Mohammed Said Issa wa ACT Wazalendo aliyesema Zanzibar inahitaji kulindwa, akidai Visiwa vimejaa Watu na wanaweza kukosa pa kuishi siku za usoni, pia alidai ajira za Wananchi wengi wa Zanzibar zimechukuliwa na wageni kama ilivyo upande wa ardhi pia