Ni kaburi la aliyekuwa SHARIFA (Kiongozi) wa kipindi Mtawala wa Zanzibar, Bwana Majid Bin Said ambaye ndiye aliyeanzisha Dar es Salaam
Kaburi hili lipo zaidi ya miaka mia mbili na lilianza kujaribiwa kuondelewa na wajerumani ikashindikana waingereza wakashindwa utawala wa Mwl.Nyerere, Mwinyi,mkapa mpaka mara ya mwisho wakati wa utawala wa Kikwete ilishindikana. Ikumbukwe eneo hilo lilikuwa na makaburi mengi lakini hilo tu ndio liligoma
NAMNA LINAVYOJILINDA
Mara kadhaa walipokuwa wanapeleka Kijiko (Excavator) au Bull dozer (Tingatinga) walikuwa wamefanikiwa kulitoboa
Lakini lilikuwa linatoa harufu kali mfano wa "SULPHUR" kutoka ndani ya Kaburi na Kufanya wanaolibomoa Kukohoa sana,Kukosa Pumzi na hata Kupoteza Fahamu
Ile harufu kali huenea eneo la Mzingo (DUARA) mpaka umbali wa mita 500 na harufu hudumu kwa ukali uleule kwa siku nyingi bila Kupungua madhara yake.
Na
Mohamed Ngangambe