Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube (27) raia wa Zimbabwe amepita njia ileile aliyopita, Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' wakati alipokuwa akishinikiza kuondoka ndani ya Yanga SC.
Dube ambaye ameshatangaza kuachana na timu hiyo, licha ya uongozi wa timu kusema kuwa bado anamkataba nao, sasa amefanya maamuzi mengine kwa kupeleka malalamiko katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya Azam FC kukataa ofa ya Tsh 510 millioni kutoka vilabu mbakimbali.
Awali ofa kama hiyo ulitolewa na Klabu za Simba SC na Al-Hilal ambapo Azam FC walizikubali ofa hizo wakaruhusu klabu zilizotoa ofa ziongee na mchezaji.
Ofa zilivyokuwa;
Tsh milioni 300 pamoja na Tsh milioni 210 ambazo baadaye wangelipa Simba SC. Tsh milioni 510 kutoka Al-Hilal ya Sudan
Prince Dube alikataa kujiunga na klabu hizo akitaka avunje mkataba awe huru ili ajiunge na klabu anayoitaka yeye.
Lakini baada ya siku chache iliarifiwa kuwa Yanga nao walituma ofa ya Tsh milioni 500 kuitaka saini ya nyota huyo ili aje kuwa mbadala wa Fiston Kalala Mayele.
Siku ya kusikilizwa shauri itatangazwa.