Kipa Beno Kakolanya Mwamba Sana, Agomea Wito wa Kamati ya Nidhamu Singida FG



Afisa habari wa @singidafountaingatefc Hussein Masanza amesema

Nahodha na Golikipa wetu, Beno David Kakolanya, amejibu barua ya wito kuwa hatoweza kufika kwenye kikao cha kamati kwa sababu anaamini kamati haitamtendea haki wakati tayari ameshatuhumiwa.

Lengo la wito wa kamati ya nidhamu lilikuwa ni kumpa nafasi ya kujibu tuhuma hizo.

Kwahiyo suala la yeye kukataa wito tunaliacha kwenye maamuzi ya kamati tuone itaamuaje.

Kakolanya alipewa barua ya wito April 15 2024 ikimtaka kufika mbele ya kamati ya nidhamu Aprili 19 2024 kujibu kuhusu kitendo cha utoro na kuhujumu timu siku chache kuelekea mechi muhimu dhidi ya Yanga SC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad