Kocha Mamelodi : Leo Tutacheza na Yanga Kama Tulivyocheza na Al Ahly



Kocha wa Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena, amesema mchezo wao wa kesho dhidi ya Yanga SC, watacheza kama walivyocheza dhidi ya Al Ahly nusu fainali ya African Football League.

Hayo ameyasema leo Afrika Kusini wakati wa maandalizi ya mchezo wao wa kesho dhidi ya Yanga SC kuwania kuingia nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tumewaona namna walivyocheza kwao na tukatoka bila ya kufungana, wana wachezaji wazuri sana kama vile Dickson Job Pamoja na Ibrahim Bacca kwenye eneo la ulinzi, lakini tutahakikisha tunapata matokeo mazuri na kuvuka.

“Nimefanya mazungumzo na mashabiki na kuwaambia mchezo huo ni kwa ajili yao lazima tupate matokeo mazuri, ninaamini tutabadilika na kucheza kama ambavyo tulicheza dhidi ya Al Ahly hatua ya nusu fainali ya African Football League hapa nyumbani.” Amesema kocha huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad