Takriban watu 60 wamekufa tangu kuanza kwa mwezi huu kutokana na mvua kubwa na mafuriko ambayo yamekumba maeneo kadhaa ya Tanzania, serikali ilisema.
Eneo la pwani la nchi hiyo ya Afrika Mashariki ni mojawapo ya maeneo yaliyoathirika zaidi, huku mafuriko yakiharibu maelfu ya mashamba huko, Mobhare Matinyi, msemaji wa serikali, alisema katika taarifa Jumapili.
"Madhara makubwa ya mafuriko yanashuhudiwa katika eneo la pwani ambapo watu 11 wamefariki kufikia sasa," Bw Matinyi aliongeza.
Alisema vifo 58 vimerekodiwa hadi sasa kutokana na mafuriko hayo.
Ijumaa iliyopita, watoto wanane wa shule walifariki baada ya basi lao kutumbukia kwenye korongo lililofurika kaskazini mwa nchi.
Aprili ni kilele cha msimu wa mvua nchini Tanzania.
Mwaka huu umeshuhudia mvua kubwa zaidi ya miaka ya hivi karibuni.
Mvua hiyo kubwa pia imesababisha vifo vya takriban watu 13 na wengine 15,000 kuyahama makazi yao katika nchi jirani ya Kenya, UN ilisema.Hali ya hewa ya El Niño imezidisha mvua za msimu wa mwaka huu, wataalam wa hali ya hewa walisema.