Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuwachukulia hatua watumishi watakaokiuka utaratibu kwa kutumia mbwa wanapowakagua abiria, mizigo na vifurushi vyenye vyakula.
Kihenzile amesema hayo leo Jumanne Aprili 16, 2024 akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Konde, Mohamed Said Issa.
Issa katika swali la nyongeza amehoji iwapo Serikali iko tayari kuwachukulia hatua watendaji wanaofanya ukaguzi kwa kutumia mbwa kwa mizigo ya abiria wanaokwenda Zanzibar kuwa ni suala la kila siku.
Amehoji Serikali inatoa kauli gani, ili jambo hilo lisijirudie. Kihenzile amemwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa TPA kuwa wanapofanya ukaguzi wazingatie utaratibu wa kutokagua abiria wala vyakula kwa kutumia mbwa.