Simba SC, kwa sasa Mashabiki na Wanachama mnachoweza kukifanya cha maana zaidi ni kuwa nyuma ya timu yenu kama kuna kambi zivunjwe, kama kuna timu zivunjwe na kama kuna makundi basi yaunganishwe, vita ni nzuri zaidi kupigana kama Unit ila sio kila Platoon inapiga kwa mipangona style yake.
NGUVU MOJA maana yake hata pale ambapo timu ipo mabondeni mnayo sababu ya kupigana irudi kileleni, kulaumu sana haitobadilisha kikosi kilichopo sasa kwakuwa dirisha limefungwa, Wachezaji hawnaa cha kufanya na Viongozi hawana cha kufanya, kinachosalia ni kusupport kilichopo mpaka mwisho mwa msimu.
Kimpira unaweza kumpa Yanga ubingwa lakini kihesabu bado Ligi haina bingwa, maaana yake ni kuiva kisaikolojia na kucheza kila mechi iliyobaki bila matarajio yoyote bali kwenda na kuonesha mlichonacho na kusubiri nini kitakuja mbele.
Niwaambie Mashabiki wa Simba, mechi zilizobaki bado ni nyingi saana! Hupaswi kuiacha timu yako hata kama Magumashi ni mengi kwakuwa Viongozi huja na kuondoka, Wachezaji huja na kuondoka ila wewe utabaki hapo daima, hii ni timu yako na hauna nyingine.
Kaa nyumbani jifungie, ukiweza lia na maliza maneno yote ila fahamu timu kwa sasa inahitaji nguvu na dua zako, namna pekee ya kuendelea kupambana ni hawa Wachezaji kusikia sauti yenu ya matarajio makubwa, huo ndio unaitwa Ushabiki.
Sumu zote, lawama na mapovu yote ni afya zaidi kuyatumia mwishoni mwa msimu! Kwasasa silaha ziwekwe chini, itazamwe timu zaidi sio watu, itazame Simba zaidi sio Wachezaji au Viongozi! Bado kuna chakula kimebaki kwenye sahani, msinawe maji na kuondoka.
Ni ukweli waliopo kwenye madaraka wanawakosea sana! Ndio wanakwama sana, ndio wanazingua sana ila nyakati hizi fumbeni kwanza macho na masikio, mwisho wa msimu ndio wakati mzuri zaidi, logo haipaswi kuwa na ukiwa! NGUVU MOJA. Kuiona Simba kwenye hii hali inasikitisha na inauma sana.